Sunday, October 7, 2012
ZAWADI TOKA KWA MUNGU
Zawadi nikitu ambacho mtu au watu hupewa pasipo kuomba na sanyingine pasipo kutarajia nini wanakwenda kupata, wakati mwingine wawezakuwa unashida na pesa kiasi lakini ukahangaika kwamuda mrefu ukashindwa kufanikisha na hatimaye waweza kata tamaa ya kupata ukitarajiacho. Mara fikiria anatokea rafiki yako mliyekuwa mnasoma nae Primary miaka mingi iliyopita na yeye tayari Mungu kambariki. Kwapamoja mkafurahi sana kwakukutana kwa mara nyingine kwani mliachana mkiwa mkingali wadogo na sasa mmekutana kila mmoja akiwa na maisha yake japo mnatofautiana kiuwezo. Akakuachia busyness card yake pamoja na maramia ya pesa ulizokuwa unahitaji pasipo kumwomba, akakukaribisha nyumbani kwake siku za weekend mkabadilishane mawazo. Furaha utakayo kuwa nayo nadhani haitaelezeka kwani umefanikiwa kupatahitaji lako tena kwa zaidi ya asilimia miamoja. Siku ya weekend ukajitahidi ukafanya mawasiliano na rafiki yako huyo, mkakutana nyumbani kwake. Mkaongea mengi sana ya kimaisha mpaka kajua kalipoanza kuzama ndio ukaomba ruhusa muagane ili uweze kurudi nyumbani kwako. Rafiki yako huyo akakusindikiza na mlipokaribia kufika katika stand ya daladala, akakuambia kuwa Jumatatu inayo fuaata ya wiki muweze kukutana katika ofisi yake na atahakikisha kuwa unapata kazi nzuri yenye mshahara mzuri. Ulibaki kinywa wazi kwakustaajabu kwani hilo kwako lilikuwa kama nindoto hasa ukizingatia shughuli zako zilikuwa za kubangaiza. Ilipofika siku ya Jumatatu ulikwenda mojakwamoja ofisini kwa rafiki yako na alikukaribisha vyema ofisini kwake na kabla ya kupoteza muda alikupa mkataba wa kazi ambayo ungetakiwa kuifanya, ulishtuka sana kwani nikazi nzuri yenye mshahara mnono ila ulikuwa huwezi kuimudu kwani ilihitaji taaluma. Kwamasikitiko ulimwambia rafiki yako kuwa unashukuru kwa msaada aliotaka kukupa ila kisomo ulichonacho hakikizi kufanya kazi kama ile. Alikutoa wasiwasi nakukuambia kuwa usijali kwani atakupeleka shule ukasomee fani ile inayohusu kazi yako tarajiwa nautakuwa unapokea mshahara haijalishi utakuwa shule na pia isitoshe shirika lake litagharamia gharama zamasomo mpaka pale utakapo maliza. Nadhani utabaki mdomo wazi nausiamini kile ambacho unaelezwa. Kama utani rafiki yako akaanza kutekeleza yale aliyokuahidi baada ya sikuchache baada ya wewe kuwa umekubali kusaini mkataba wa shirika lake.
Mfano huo ni sawa na upendo wa Mungu wetu kwetu kwakutupa yale tusiyotarajia, mpaka muda mwingine huwa na mshangaa sana Mungu, hebu fikiria anakupa zawadi ya mtoto au watoto, tena muda mwingine anakubariki nakukupa watoto wenye viungo sawa na akili timamu. Tena zaidi yahapo anazidi kukubariki na kuwafanya watoto wako wawe wasikivu kwako na watii kwa wakubwa na kushika mafunzo ya darasani na ya Biblia. Mungu anaendelea kubariki zaidi ya ulivyokuwa ukitegemea. Nivyema tupewapo zawadi tukarudi kushukuru, Mungu wetu ni mwema daima na sikuzote yeye amtegemeae hata aibika. Tuwalee watoto wetu vizuri katika misingi mizuri kwani wakiharibikiwa mbele yasafari yao wakulaumiwa utakuwa ni wewe mzazi kwani umeshindwa kuienzi zawadi bora toka kwa Baba. Daima tuwaombee watoto wetu na tuwaelekeze kwa upole nini wanatakiwa wafanya nanini wasifanye bila kusahau kudumu katika maombi na ikiwezekana wakikuwa wakubwa uwafundishe kutoa neno nyumbani na uwafanye wampende nakumwogopa Mungu.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nayi nyote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Katika hali ya kumpenda Mungu baba hatuna budi kushukuru kwa kila jambo atutendealo, halijalishi nilipi. Mungu wetu ni mwema daima na yeye hutuwazia mazuri sikuzote, nasi twapaswa kuwa na moyo wa shukrani.
ReplyDeleteMungu Baba ni muweza na hakika tukimkiri Mwanae yesu Kristo yakuwa ni Mwana wa Mungu hakika tutauona ufalme wa Mungu napia tuzingatie mafundisho yake.
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHizi post ni nzuri sana na zinabariki, asante sana na uzidi Kubarikiwa mtumishi!
ReplyDeleteHakika ubarikiwe sana mtumishi!!
ReplyDeletesikuhizi mtumishi mbona hutukumbuki kwa mafunzo yako?
ReplyDelete