Mazingira ya sehemu ya utafutaji riziki huwa na majaribu yakila aina, kama ni maofisini pia hakutakuwa shwari sikuzote, kama ni shambani pia huko nako kwaweza kuwa na magumu ya ainayake. Katika biashara pia nako kwaweza kuwa na magumu yake na katika shughuli yoyote ndani ya jamii hujitokeza mambombalimbali ambayo huchangia kwa namnamoja amanyingine tuweze kata tamaa. Shetani na wafuasi wake anaweza kusababisha magumu kupitia kwa watu wako wa karibu au hata wafanyakazi wenzako, nia namadhumuni niwewe uweze kukata tamaa nakuanguka. Bila ulinzi wa Mungu kamwe hatutaweza, silaha yetu ni maombi. Katika maombi tunapata ushindi, kamwe hatutashindwa iwapo tutamtegemea Mungu katika roho na kweli.
Nasema hayo kwani yalisha wahi kunikuta hata na mimi katika mazingira ya utafutaji wa mkate wa kila siku, ilifikia mpaka wakati nikakata tamaa kabisa. Lakini dada yangu mpendwa alinipigia simu nakuniambia, nisikate tamaa kwani MUNGU wetu hashindwi kamwe, akanieleza kuwa nisome Zaburi ya 70 na siku chache nitaona majibu. Kwli nilisoma Zaburi ya 70 usiku kabla sijalala na asubuhi kabla sijakwenda kazini kwangu. Majibu hayakuchukua muda mrefu nikaona mambo yamesawazika na kuwa kama kawaida. Nilipata furaha sana na mpaka sasa hivi siwezi kutoka chumbani kwangu asubuhi kabla sijaisoma Zaburi ya 70 na hata pia siwezi kulala kabla sijaisoma Zaburi ya 70. Hakika mambo yangu sasa yananiendea vyema si kama mwanzo mpaka nikakata tamaa.
Zaburi 70
1 Ee Mungu, uniokoe, Ee Bwana, unisaidie hima.
2 Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
3 Warudi nyuma, na iwe aibu yao, Wanaosema, Ewe! Ewe!
4 Washangilie, wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, Atukuzwe Mungu.
5 Nami ni maskini na mhitaji, Ee Mungu, unijilie kwa haraka. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Bwana, usikawie.
No comments:
Post a Comment