Bwana Yesu Asifiwe.
Mimi huwa nafikiri jambo hili nijema pindi tunapotaka kusali kuzingatia:
Kuomba utakaso wa makosa ambayo tumeyatenda eidha katika kufikiri, kutenda ama kunena. Kwani tukisema kuwa hatuna dhambi twajidanganya wenyewe nawala kweli haipo kwetu. Tukumbuke kuwa pindi tunapotaka kusali tunakwenda kuongea na MTAKATIFU, hivyo nibora tukajitakasa ili iwe rahisi sala zetu ziweze kusikilizwa. Baada yakuomba utakaso ndipo unaweza kuendelea na maombi yako. Pia kabla ya kuomba nibora ujiandae kifikra kwani unakuwa unataka kuondoa mawazo ya kiulimwengu nakuhitaji kuongea na mtakatifu zaidi, ndiomaana wengi hupendelea kabla ya kuzama katika maombi huanza na nyimbo za sifa nahatimaye nyimbo zakuabudu ndipo huingia katika sala, mpenzi wa blogu yangu nakwambia kuwa tukifuata utaratibu mzuri wa kusali, hata yule anayezuia maombi yetu, yaani mkuu wa anga hataweza kufanya hivyo. Wengi wetu bila nyimbo za sifa au zautulivu, tunaingia katika maombi na sanyingine tunaomba mahitaji bila kuomba utakaso kwanza, unajiuliza mbona maombi yangu hayajibiwi, lakini kumbe tunaomba vibaya. Tukifuata utaratibu mzuri ninaamini twaweza kujibiwa aombi yetu, najua kuwa tunamajukumu mengi ya kutafuta mkate wa kila siku lakini nivyema baada ya shughuli ya kutwa nzima ili kuepuka kuomba ukiwa umechoka, nenda bafuni kaoge ili utoe uchovu ulionao kisha jiandae kifikra kuongea na MUNGU wako. Baada ya kuomba utakaso, mshukuru kwa kukulinda kutwa nzima kwani amekuepusha na mabaya mengi huenda bila ulinzi wake ungepatwa na mabaya. Baada yahapo omba hitaji lako unalotaka kutoka kwake halafu ombea na wenzako ili nao wawezepata baraka, kumbuka wenyeshida mbalimbali katika maombi yako ili Bwana aweze kuwafungua ili jina lake lizidi kuhimidiwa, kuna watoto yatima, wajane, walioondokewa na wapendwa wao, wasafiri, wafungwa na walio katika vita hasa watoto na wamama ambao ndio wahanga wakubwa katika misukosuko. Ombea wanao hubiri NENO la MUNGU, ili watumiwe kama chombo na maneno yao yakaweze kupata mavuno mazuri na mengi. Kwani kwake yeye twapata nguvu na tunaweza kuomba lolote kwajina lake natukapewa. Baada ya hapo shukuru, vunja nguvu za ibilisi Shetani na maajenti wake kupitia lile jina lipitalo majina yote yaani YESU KRISTO, kwani hilo jina likitajwa kuzimu amani inatoweka kabisa na linasambaratisha mipango yote mibovu ya ya shetani na maajenti wake. Chamsingi zingatia unapoomba uzame katika ulimwengu wa roho, ukiwa katika maombi ukaona unakumbuka mambo ya duniani miyayo mingi hujisikii kusali bali unajilazimisha na unaona unachelewa kulala unasali tu ilimradi kutimiza sheria wala hutilii maanani katika unalofanya, hiyo ndugu yangu haitaweza kusaidia, jitahidi kumweshimu MUNGU hususani pindi unapotaka kuongea nae, usipo onyesha consecrations katika maombi utakuwa unafanya kazi bure. Hebu mfano chukulia unamtoto ambaye hupenda kufanya mazoezi, sasa akiwa anaongea narafiki yake maneno yautani na hapohapo akakuona unapita karibu ukiwa na shughuli zako, pasipo kukusalimia na kuonyesha umakini wowote ule, anakwambia 'baba viatu vya mazoezi' na baada yakutamka hayo anaendelea kuongea na rafiki yake pasipo kutilia maanani ya nini anahitaji. Nadhani baba hata jua nivipi unahitaji viatu vya mazoezi kwa kiasi gani, matokeo yake hata tilia maanani katika maombi ya viatu vya mazoezi. Lakini mtoto akiwa amjipanga vyema na kujiandaa kwenda kuomba viatu vyamazoezi kw babaye, kwaunyenyekevu na nidhamu tena kwa machozi, akisema baba tizama miguu yangu imeharibiwa na miiba ona vidonda vyangu hivi miguuni, vinanitesa sana baba yangu, naumia baba, naomba unisaidie unipatie pesa ya kununulia viatu ili nisiumie zaidi baba yangu mpendwa. Naamini baba yangu unanipenda na haupo tayari kuniona mwanao nataabika kiasi hiki, nakuomba kwa upendo wako baba yangu unitimizie haja yangu hii. Naamini baba atamwonea huruma mtoto wake nakununulia au kumpa pesa mwanae ili aweze kununua viatu na asiumizwe na miba tena pindi afanyapo mazoezi.
Bwana Yesu awe nasi sote. Amani ya Mungu ipitayo fahamu zote ikulinde na kukubariki katika hali ya kumjua na kumpenda MUNGU siku zote za maisha yako.
No comments:
Post a Comment