Thursday, October 18, 2012
DAKIKA TANO TU!
Bwana Yesu asifiwe,
Naomba uniruhusu niliseme hili jambo kidogo japo wengi wetu huwa hatulitilii maanani. Hivi ulishawahi kujiuliza maswali haya yafuatayo? rafiki yangu amefariki je!amekwenda wapi? au baada ya kumzika ndo amekuwa mbolea ya aridhi na ndo mwisho wa hadithi yake? Kama ndivyo udhaniavyo bila shaka upo sawa kulingana na fikra zako zinavyo kutuma. Nawengi bila shaka walikuwa na fikra zanamna hii enzi zile za ujinga ndo maana Yesu aliwatuma wanafunzi wake wakaihubiri injili kwakila kiumbe ili aaminiye na kubatizwa aokolewe bali atakayekataa atahukumiwa Marko 16: 15.
Sivizuri mtu kufa na dhambi zake wala haipendezi, hebu fikiria unakufa ukiwa unaamini kuwa hakuna Mungu, mahubiri yanafundishwa lakini hutaki kubadilika unang'ang'ana na msimamo wako wa hakuna Mungu na ukifa unatimiza moja ya sifa ya kiumbe hai. Hivi ndio unatangulia mbele za haki halafu unakutana na malipo unayo stahili huko sijui utaomba udhuru kidogo ili ukatubu! itakuwa too late. Muda wa kutengeneza ni sasa nawala si kesho, makazi yetu sisi ya kudumu si hapa. Hebu jiulize marafiki zako wangapi hawapo wamesha tangulia? unajua walipo hivi sasa? wamekuwa mboji? Nakwambia mtu akitoka kuzimu akapata wasaa walau wa nusu saa ya kurekebisha utashangaa atakavyo kuwa na bidii ili asirudi alikokuwa. Lakini muda wake unakuwa tayari umeshapita na huo ndo ujira wa maisha yake aliyokuwa anaishi nayo duniani. Sisi tulio hai ndo tunawasaa mzuri wakutengeneza maisha yetu ili tuukwepe moto na mateso ya kuzimu kwani nivilio tupu vimejaa huko na uchungu usio elezeka.
Hujui utaitwa lini mbele ya haki, lakini nivyema kujitakasa sana ili tusiwe na madoadoa, wapo baadhi ya watu wanania mbili, anapenda wokovu halafu upande mwingine anapenda dunia na mambo yake yaliyo chukizo mbele za Bwana. Nibora kama mtu ameamua kuokoka na kumpa Bwana maisha yake, aache nawala asifikiri kurudi njia ya upotevuni. Na ambaye anafanya dhambi azidi kufanya dhambi ili siku ya mwisho aweze pata stahiki yake ya halali. Mwenzangu na mimi uliyekuwa unapenda huku na kule huoni kuwa utakuwa umepunjika? Kwani huwezi kupenda mabwana wawili kwani unaweza kumpenda yule na kumchukia yule. Nasivyema kuwa vuguvugu kwani utakuwa huna unalo lifanya na utatapikwa.
Maombi yawe ni silaha yetu, mpenzi msomaji wa blogi hii nakwambia kuwa hakuna raha kama ukiwa unawasiliana na Mungu wako mojakwamoja, Shetani kamwe hataweza kukugusa na utakuwa salama katika mikono salama ya Bwana Yesu.
Mungu atusaidie sana ili tuweze kufikia ile ahadi tuliyo ahidiwa.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nasi sote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment