Binti mdogo kama huyu akilelewa katika misingi imara ya dini ya Kikristo, hofu ya MUNGU ikajengwa ndani yake maadili mema yakaanzwa katika msingi wa umri kama huu, hakika maisha yake yatakuwa nimfano wa kuigwa na jamii yenye ustaarabu. Lakini binti huyuhuyu akilelewa katika maisha yasiyo na msingi wa Kikristo, hofu ya Mungu isiwe ndani yake na maadili yakapita kushoto kwake ninaamini kuwa binti huyu atakuwa ni binti hatari na asiyetakiwa katika ulimwengu wa kistaarabu kwani Shetani aweza mtumia katika mipango yake ya kudhoofisha kanisa la Bwana.
Ninamaana nzuri tu kutoa utangulizi wa jinsi hiyo. Kanisa huanzia nyumbani, baba, mama pamoja na watoto wakiwa wanadumu katika sala, baraka za MUNGU BABA hufunika nyumba hiyo kwakiwango kikubwa ajabu na baraka humiminika. Lakini nyumba ikiwa imefunikwa na hirizi pamoja na tunguri, mwisho wake huwa unakuwa ni laana tupu. Ninamfano ulio hai, kaka yangu mmoja kipindi nakuwa nilimweleza azoeshe wanae kwenda kanisani kwani si vyema neno la Mungu mkristo asilijue. Alipuuza ushauri wangu, baadae nilikuja kugundua kuwa nyumba yake ilitawaliwa na nguvu za giza kwani kila kona kulikuwa na hirizi kwaajili ya kuwalinda. Matokeo yake sasa, mkewe kuzini nje ya ndoa si shida kadhalika na yeye kutoka nje ya ndoa haoni ni kosa, matokeo yake sasa binti wake wa kwanza aliyekuwa kidato cha pili kesha zalia nyumbani na maisha yanaendelea mbele. Madeni mkewe aliyokopa ameshindwa kuyalipa na kampuni za ukopeshaji zimewafilisi kwa kubeba aseti zao za ndani.
Nataka kumalizia kuwa kumcha Bwana ni jambo zuri sana, kufuata maagizo yake ni jambo zuri sana. Braka za Mungu zitakutangulia uamkapo, ulalapo na popote utakapo kuwa baraka za Mungu zitakuandama. Bali ukimwacha Bwana tayari unakuwa umelaaniwa Yeremia anathibitisha hilo. Tuwalee vyema watoto wetu katika kito cha Bwana Mungu hakika utakujakuwa na familia bora sana na yenyekupendeza. Waefeso6. Bwana awe nanyi daima na atuwezeshe kuwalea watoto wetu vyema ili laana ituepuke tusiwe kama Eli alivyo laaniwa kwasababu ya watoto wake.
No comments:
Post a Comment