Eeh, Mwenyezi Mungu. Nakushukuru kwa kunilinda mchana kutwa, umenikinga dhidi ya majanga mbalimbali ambayo yalikuwa yakinikabili, eidha mengine kwa kuyaona au pasipo kuyaona na kutambua.
Nakuomba unisamehe pale nilipo kukosea, eidha katika kunena, kutenda nahata kuwaza. Nisamehe Mungu wangu na unioshe kwa damu ya mwanao Yesu Kriso aliyo imwaga pale msalabani ili nipate kukombolewa. Nakuomba ee Mungu wangu unilinde dhidi ya hila zote za mwovu. Malaika wako walinde nyumba yangu kwa moto ulao, funika nyumba yangu dhidi ya uovu waaina yoyote ile. Pia Mungu wangu nakuomba kesho niamke nikiwa salama mimi pamoja na wote walio katika nyumba hii, tuwe na ari ya kukupenda, kukutukuza na kulihimidi na kulitangaza jina lako ili watu wengine waokolewe. Tujalie afya njema, wape nguvu wagonjwa pia bariki wanao wauguza ili wawauguze kwa upole na kwa unyenyekevu, wakumbuke wafungwa, wajane, wasafiri na wenye mahitaji mbalimbali. Navunja na kuharibu nguvu za giza, nikatika JINA LA YESU zikashindwe na kuharibika. Pia watumishi wako nawaweka mikononi mwako ili wakatumiwe na wewe kama chombo chakufikisha neno lako ili mavuno yatakayo patikana yakawe kwaajili ya sifa na utukufu wako.
Naomba nakuamini ni katika Jina lipitalo majina yote la Yesu Kristo. Amin.