KUANGUKA NA KURUDI NYUMA
Ndugu, tukisema yakuwa hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, nawala kweli haimo mwetu kabisa. Shetani huzunguka hukuna huku, yupo busy kwelikweli kuhakikisha kuwa hakuna mteule yeyote atakaye weza kuurithi ufalme wa Mungu. Huyu kiumbe ni waajabu sana, anawivu uliokithiri, sasa mimi nikiurithi huo uzima wa milele yeye anapungukiwa nini? saanyingine nikizitafakari shughuli za ibilisi hapa duniani, napatwa na hasira sana dhidi yake, ila vita vyetu tunavyopigana si vya mwili na damu bali ni vya kiroho, na silaha kubwa ni MAOMBI. Mpendwa bila maombi katu hatutaviweza vita hivi vyakiroho, shetani anambinu nyingi mno. Tusipo omba ulinzi wa MUNGU nidhahiri kuwa nilazima tutaanguka, hatuna budi kujizatiti kiimani na KUMKIRI YESU KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WETU, hili ndio jina ambalo shetani huliogopa na kukaa mbali nalo, kuzimu ni mwiko kulitaja jina la YESU, sasa kwakuwa mapepo wanaliogopa nivizuri kulitumia ili kujilinda na hayo madudu yenye nia mbaya nasi, Jina la YESU tulitumie kama upanga na zaidi tusome biblia na kuielewa vyema. Tukumbuke ile amri kuu tuliyo achiwa ya UPENDO, pia tukumbuke kuifuata ile dini tuliyo ambiwa ni nzuri ambayo ni ile ya KUWAJALI WAJANE NA WATOTO YATIMA. Na zaidi tupende kumjua yeye na kuzishika amri zake.
Mfano: Nilikuwa naishi mbali na familia yangu kutokana na mazingira ya kazi ninayoifanya, ndiomaana imepelekea mimi kuwa mbali na familia yangu, sa nyingine na maliza mwaka kuwa mbali na mke wangu na watoto wangu, nilikuwa napata wakati mgumu sana wa kuweza kuucontrol mwili lakini ilinibidi kuhakikisha kuwa mambo hatokwenda kombo. Nilijitahidi sana kwakweli kumlindia heshima mke wangu. Mambo yaliharibika baada ya binti ambaye alikuwa ni mfanyakazi mwenzetu kujenga mazoea ya kuwa karibu na mimi, nilijikuta nikimwambia nahitaji kufanya upuuzi na yeye, bila hiana nayeye akakubali, nilijuta sana kwa kitendo kile lakini, hapo shetani amesha faulu kukukamata na kukuweka katika himaya yake na katu hufurukuti.
Mfano huu nidhahiri kuwa kunakitu hapa kilipungua, Kuomba ulinzi wa MUNGU, kuepuka tamaa mbaya za mwili, hofu ya MUNGU ilikuwa mbali ndo maana hiyo dhambi ya uzinzi ilifanyika.
Mungu atuhurumie sana na atupe ulinzi wake na hekima yakuweza kugundua mitego ya huyu mwovu asiyetutakia mema kila kukicha!!