Ninamshukuru Mungu kwa Neema zake, Mwaka juzi nilipatwa na makamasi ya ajabu sijawahi kuona katika maisha yangu, ilikuwa hivi! sikumbuki mwezi gani ila ni mwaka 2007 sikujua yalianza vipi nilikuwa sina kifua au kukohoa nilishtukia tu nina makamasi ya ajabu mno, yalinitoka bila kujua kama yanatoka wala nini halafu mazito mno kama Uji (samahani kwa hilo) pia yalinuka sana sikuweza kutumia kitambaa cheupe maana yalikuwa na rangi ya njano sijui hata niseme njano ipi jamani, nilikosa raha ya kuishi Marekani maana kila wakati yanatoka bila mimi kujua.
Pia pua moja haikufanya kazi yaani kama natoa moja naiziba halafu ndo natoa. Nilikuwa sijamjua Mungu kabisa ila baadae nikaona yanazidi kunuka na kunipa shida nikipanda Train ilikua kero kwangu mpaka nifiche pua, sasa wakati mwingine ni summer so nilikuwa siwezi kufanya hivyo, kipindi cha winter sawa nakuwa nafuu kidogo, nikaanza kuomba na kufunga bado haikusaidia, sikukata tamaa nimekaa miaka miwili nikarudi Tanzania nikawa bado tu siku moja nikawa natokwa na makamasi sikuwa na kitambaa ikabidi niombe kwa mtu ambaye nilikua nae akawa hana, akanipa kile kile alichotumia yeye nikasema sawa nipe tu, nikajisemea moyoni hali hii itaisha lini?
Kile kitambaa nikatumia na kutupa, niliona aibu rangi ya kamasi, khanga zote ziliharibiwa kwa hilo, sasa basi mwaka huu wakati nakaribia kurudi Marekani sikumbuki makamasi yaliisha lini, nikawa natoa kamasi meupe kama sufi mh nikasema ehh ina maana yamekwisha yale ya ajabu!!!
Mpaka leo hii nipo mzima kabisa, namshukuru Mungu sana kwa kuniponya maana ilikuwa kero sana na harufu kali sana sasa leo ni mzima kabisa, Mungu atukuzwe kwa hilo. AMEN