Friday, December 7, 2012

KUANGUKA NA KURUDI NYUMA
Ndugu, tukisema yakuwa hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, nawala kweli haimo mwetu kabisa. Shetani huzunguka hukuna huku, yupo busy kwelikweli kuhakikisha kuwa hakuna mteule yeyote atakaye weza kuurithi ufalme wa Mungu. Huyu kiumbe ni waajabu sana, anawivu uliokithiri, sasa mimi nikiurithi huo uzima wa milele yeye anapungukiwa nini? saanyingine nikizitafakari shughuli za ibilisi hapa duniani, napatwa na hasira sana dhidi yake, ila vita vyetu tunavyopigana si vya mwili na damu bali ni vya kiroho, na silaha kubwa ni MAOMBI. Mpendwa bila maombi katu hatutaviweza vita hivi vyakiroho, shetani anambinu nyingi mno. Tusipo omba ulinzi wa MUNGU nidhahiri kuwa nilazima tutaanguka, hatuna budi kujizatiti kiimani na KUMKIRI YESU KUWA NI BWANA NA MWOKOZI WETU, hili ndio jina ambalo shetani huliogopa na kukaa mbali nalo, kuzimu ni mwiko kulitaja jina la YESU, sasa kwakuwa mapepo wanaliogopa nivizuri kulitumia ili kujilinda na hayo madudu yenye nia mbaya nasi, Jina la YESU tulitumie kama upanga na zaidi tusome biblia na kuielewa vyema. Tukumbuke ile amri kuu tuliyo achiwa ya UPENDO, pia tukumbuke kuifuata ile dini tuliyo ambiwa ni nzuri ambayo ni ile ya KUWAJALI WAJANE NA WATOTO YATIMA. Na zaidi tupende kumjua yeye na kuzishika amri zake.
Mfano: Nilikuwa naishi mbali na familia yangu kutokana na mazingira ya kazi ninayoifanya, ndiomaana imepelekea mimi kuwa mbali na familia yangu, sa nyingine na maliza mwaka kuwa mbali na mke wangu na watoto wangu, nilikuwa napata wakati mgumu sana wa kuweza kuucontrol mwili lakini ilinibidi kuhakikisha kuwa mambo hatokwenda kombo. Nilijitahidi sana kwakweli kumlindia heshima  mke wangu. Mambo yaliharibika baada ya binti ambaye alikuwa ni mfanyakazi mwenzetu kujenga mazoea ya kuwa karibu na mimi, nilijikuta nikimwambia nahitaji kufanya upuuzi na yeye, bila hiana nayeye akakubali, nilijuta sana kwa kitendo kile lakini, hapo shetani amesha faulu kukukamata na kukuweka katika himaya yake na katu hufurukuti. 
Mfano huu nidhahiri kuwa kunakitu hapa kilipungua, Kuomba ulinzi wa MUNGU, kuepuka tamaa mbaya za mwili, hofu ya MUNGU ilikuwa mbali ndo maana hiyo dhambi ya uzinzi ilifanyika.
Mungu atuhurumie sana na atupe ulinzi wake na hekima yakuweza kugundua mitego ya huyu mwovu asiyetutakia mema kila kukicha!!


Friday, November 2, 2012

Luka 15



1  Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize.
2  Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.
3  Akawaambia mfano huu, akisema,
4  Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
5  Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.
6  Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.
7  Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.
8  Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
9  Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
10  Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
11  Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili;
12  yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake.
13  Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.
14  Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji.
15  Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
16  Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.
17  Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
18  Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;
19  sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.
20  Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.
21  Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena.
22  Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;
23  mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi;
24  kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.
25  Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.
26  Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?
27  Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima.
28  Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi.
29  Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
30  lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.
31  Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako.
32  Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.

Thursday, November 1, 2012

1 Wafalme 13



1  Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba.
2  Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.
3  Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.
4  Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena.
5  Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana.
6  Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.
7  Mfalme akamwambia mtu wa Mungu, Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakupa thawabu.
8  Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa;
9  maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la Bwana, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.
10  Basi akaenda zake kwa njia nyingine, wala hakurudi kwa njia ile aliyoijia Betheli.
11  Basi nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; na wanawe wakamwendea wakamwambia kila neno alilolitenda yule mtu wa Mungu siku ile katika Betheli; na maneno aliyomwambia mfalme, hayo nayo walimwambia baba yao.
12  Baba yao akawaambia, Amekwenda zake kwa njia ipi? Kwa maana wanawe walikuwa wameiona njia ile aliyoiendea yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda.
13  Akawaambia wanawe, Nitandikieni punda. Wakamtandikia punda, naye akampanda.
14  Akamfuata mtu wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda? Akamwambia, Mimi ndiye.
15  Akamwambia, Karibu kwangu nyumbani, ule chakula.
16  Naye akamwambia, Siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala sinywi maji pamoja nawe hapa;
17  kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.
18  Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
19  Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake.
20  Hata ikawa, walipokuwa wameketi mezani, neno la Bwana likamjia nabii yule aliyemrudisha;
21  akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, Bwana asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya Bwana, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru Bwana, Mungu wako,
22  bali umerudi, ukala chakula ukanywa maji, hapo alipokuambia, Usile chakula, wala usinywe maji; maiti yako haitaliingia kaburi la baba zako.
23  Basi ikawa, alipokwisha kula chakula na kunywa maji, yule nabii aliyemrudisha akamtandikia punda.
24  Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti.
25  Na tazama, watu wakapita, wakauona mzoga umetupwa njiani, na yule simba akisimama karibu na mzoga, wakaenda, wakatoa habari katika mji ule alimokaa yule nabii mzee.
26  Na yule nabii aliyemrudisha njiani alipopata habari, akasema; Ndiye yule mtu wa Mungu, aliyeiasi kauli ya Bwana; kwa hiyo Bwana amempambanisha na simba, simba akamrarua, akamwua, sawasawa na neno la Bwana alilomwambia.
27  Akawaambia wanawe, akasema, Nitandikieni punda. Wakamtandikia.
28  Akaenda, akamwona yule maiti ametupwa njiani, na punda na simba wamesimama karibu na maiti; yule simba alikuwa hakumla maiti, wala hakumrarua punda.
29  Nabii yule akamtwaa maiti wa yule mtu wa Mungu, akamweka juu ya punda wake, akamrudisha; yule nabii mzee akaenda mjini mwake, kukaa matanga, na kumzika.
30  Akamweka maiti katika kaburi lake mwenyewe; wakamlilia, wakisema, Aa! Ndugu yangu!
31  Hata ikawa, alipokwisha kumzika, akawaambia wanawe, akasema, Nikifa mimi, nizikeni katika kaburi hili alimozikwa yule mtu wa Mungu; iwekeni mifupa yangu kando ya mifupa yake.
32  Kwa maana neno hilo alilolia juu ya madhabahu katika Betheli, kwa neno la Bwana, na juu ya nyumba zote za mahali pa juu zilizo katika miji ya Samaria, hakika litatimizwa.
33  Baada ya hayo Yeroboamu hakuiacha njia yake mbovu, lakini akafanya tena makuhani wa mahali pa juu, wa watu wo wote.
34  Kila aliyetaka akamfanya wakfu, ili wawepo makuhani wa mahali pa juu. Jambo hilo likawa dhambi kwa nyumba ya Yeroboamu, hata kuiharibu, na kuifuta usoni pa nchi.

Thursday, October 25, 2012

KITABU CHA BIBLIA


MWANZO
1. Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2. nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lili­kuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. (MWA 1:1-3)
Jina la kitabu kwa Kilatini ni GENESIS, maana yake ni kuzaliwa, mwanzo. Tafsiri zingine zinatumia majina ya Ki­latini: GENESIS. Na zingine: KITABU CHA KWANZA CHA MUSA. Biblia ya Kiswahili inatumia jina: MWANZO. Kiebrania kitabu hiki kinaitwa BERE´SHIT. Maana yake ni Mwanzoni.
Kitabu kinatueleza mwanzo wa mambo yote isipokuwa Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu. Wao hawana mwanzo. Ndani ya kitabu hiki kuna mianzo mingi. Kwa mfano: kuna mwanzo wa uli­mwengu, mwanzo wa taifa la wana­damu, mwanzo wa dhambi ulimwe­nguni. Kuna mwanzo wa ahadi ya ukombozi. Na pia mwanzo wa maisha ya familia. Mwanzo wa ustaarabu wa wanadamu na mwanzo wa mataifa ya ulimwengu. Na pia mwanzo wa taifa la Wayahudi yaani mwanzo wa taifa la Waebrania.
Kitabu cha MWANZO kinaeleza wo­kovu pia lakini kwa kutumia mifano. Kwa mfano: Kuingia katika safina kabla ya mafuriko.
Shetani anachukia zaidi kitabu cha mwanzo na mwisho wa Biblia. Yaani MWANZO na UFUNUO. Kwa nini anachukia MWANZO? Kwa sababu inatangaza ukuu wa Mungu, uadui kati ya Shetani na Mungu na udanganyifu wa Shetani kwa wanadamu. Kitabu kinatanga­za hukumu kwa Shetani.
14. Bwana akamwambia nyoka, Kwa sababu umeya­fanya hayo, umela­aniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; 15. nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. (MWA 3:14,15)
Kwa ajili ya hayo Shetani anachukia vitabu vya MWANZO na UFUNUO. Shetani anajua kwamba baadaye uzao wa mwanamke utamponda kichwa. Maana yake ni: Yesu atamshinda Shetani kabisa.
26. Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia na kumi; wakampaka dawa, wa­kamtia katika sanduku, huko Misri. (MWA 50:26)
Kitabu cha MWANZO huanza na Mungu, la­kini kinamalizikia katika sanduku la ku­zikia maiti.
Kitabu hiki ni historia ya kushindwa kwa mtu. Lakini tunaona kwamba kila mara mtu ali­poshindwa Mungu alikuwapo kumwo­koa. Yeye ni Mwokozi wa ajabu.
Muda wa MWANZO: Kuanzia tangu mwanzoni mpaka elfu moja mia nane (1800) kabla ya Kristo.
KUTOKA
1. Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pa­moja na Yakobo. (KUT 1:1)
Katikati ya MWANZO na KUTOKA kuna miaka mia mbili na hamsini. Wakati huo Biblia imenyamaza kimya. Wakati huo taifa la Israeli waliongezeka huko Misri toka watu kama mia moja hadi watu milioni mbili hadi tatu.
Kitabu cha KUTOKA kinaitwa Kilatini: EXO­DUS. Maana yake: Kuondoka, Toka nje, Kwenda, Maandamano wa kuondoka. Tafsiri zingine zinatumia jina: EXODUS, au KITABU CHA PILI YA MUSA, au kama tafsiri ya Kiswahili: KUTOKA.
KU­TOKA ni kitabu cha ukombozi kina­chotueleza kuokoka kutoka wapi, ina­wezekanaje na mwanadamu anaokoka kwenda wapi? Anaokoka kutoka utumwa wa Misri ana­toka kupitia damu ya mwanakondoo wa pasaka, anapita Bahari ya Shamu. Ni mfano: mtu anaokoka kutoka dhambi. Kupita Bahari ya Shamu ni mfano wa ubatizo. (1KOR 10:1,2). Ni mifano ya mambo ya Agano Jipya. Na baadaye mtu ana­tembea jangwani kue­lekea nchi ya ahadi.
Mungu alitaka akae kati ya watu wake na kwa ajili ya hii akawaamuru wajenge Hema ya kukutania. Muda wa KUTOKA: 1558-1447 K.K.
Musa alizaliwa 1528 K.K.
MAMBO ya WALAWI
Kitabu kimeandikwa mara baada ya mwanzo wa safari jangwani, hema ya kukutania ilipokamilika. Hema ya kukutania ilikamilika mwaka wa elfu moja mia nne arobaini na saba kabla ya Kristo. (1447). Jina la kitabu kwa Kilatini ni LEVITICUS, maana yake ni: Kinawahusu Walawi. Tafsiri zingine zinaitwa: KITABU CHA TATU CHA MUSA. Au MAMBO YA WALAWI, kama tafsiri ya Kiswahili.
MAMBO YA WALAWI ni kitabu cha uta­kaso. Maana ya utakaso au kutakasa ni kufanya takatifu au kutangaza au kutambua hali ya utakatifu. Shule ya utakaso inaanza kwa kujifunza dhabihu. Bila dhabihu huwezi kujita­kasa.
1. Bwana akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia, 2. Nena na wana wa Israeli, uwaambie, mtu wa kwenu ata­ka­pomtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng´ombe na ka­tika kondoo. (LAW 1:1,2)
Mwanzoni mwa kitabu hiki kuna dhabihu kuu tano:
- Kwanza ni Sadaka ya kuteketezwa. Sadaka ya kuteketezwa ni mfano wa Kristo, ambaye ... alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa. (EBR 9:14).
- Pili: Sadaka ya Unga ni mfano wa Yesu Kristo aliyechu­kua ubinadamu mbele ya watu na ya Mungu.
- Tatu: Sadaka za amani ni mfano kwamba ku­pitia Yesu sisi tuna mawasiliano na Mungu.
- Nne: Sadaka ya dhambiSadaka ya dhambi ni sadaka kwa Wakristo wanyo­nge. Na anayejua yeye si Mkristo mkamilifu bali dhambi ikaayo ndani yake. Paulo alisema hivi Warumi, sura ya saba, mstari wa kumi na saba. Hatutasoma.
- Tano: Sadaka ya hatia ni mfano kwa Kristo kwa wasioa­mini, anayetafuta wokovu. Nasadaka ya hatia ni pia Kristo kwa Mkristo aliyeanguka dhambini lakini anayetaka kurudi.
Kitabu hiki kimeandikwa 1447 K.K.
HESABU
Kitabu hiki kwa Kilatini ni NUMERI. Kwa tafsiri nyingine ni HESABU, MAHESABU, au KITABU CHA NNE CHA MUSA. Jina hili ni kwa sababu ya hesabu zilizoko kwenye kitabu hiki.
Watu wa Israeli walihe­sabiwa wakati wa kwenda jangwani. Kitabu hiki kinaeleza juu ya safari ya wana wa Israeli na vita vilivyotokea wakati ule na ushindi waliopa­ta. Kwetu sisi kitabu hiki ni mwongozo wa safari. Mambo yanayofana­na na haya yanakuwepo katika maisha yetu.
Kitabu hiki kinachukua muda wa karibu miaka arobaini. Yaani kama 1446-1408 K.K.
1. Bwana akanena na Musa katika bara ya Sinai, he­mani mwa kukuta­nia, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri, akamwambia, (HES 1:1)
Kitabu kinaanza kwa kusikiliza mazu­ngumzo ya Mungu. Kama vile Musa alivyokwendahemani mwa kukutania, na Bwana akanena na Musa, vivyo hivyo ni muhimu sisi pia kumsikiliza Bwana anaponena nasi. Hapo ndipo katika safari yetu, na vita tuna­vyoyakutana navyo, tunaweza kushinda na baadaye tukafika mbinguni.
13. Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo Bwana aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko. (HES 36:13)
Hapo walikuwepo karibu na nchi ya Israeli. Kitabu hiki ni mwongozo wa safari. Itakapoanza kusikiliza maneno ya Bwana, safari yetu ni nzuri.
KUMBUKUMBU LA TORATI
Kitabu kinaitwa kwa Kilatini DEUTERO­NIMIUM. Kwa tafsiri nyi­ngine: Sheria ya pili, Na­kala au Kitabu cha tano cha Musa. Kitabu cha ukumbusho.
19. Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama Bwana, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea. (KUM 1:19)
Hapa yanakumbukwa yale yaliyotokea wa­kati wa safari. Na pia kuna maagizo mbali mbali. Ni mfano kwetu jinsi gani baada ya safari (HE­SABU) tutakavyoingia katika umi­lele na tunapitia yale tuliyoyaona wakati wa maisha yetu. KUMBUKUMBU LA TORATI ilitokea kama mwaka wa 1408 K.K.
Kitabu cha YOSHUA
1. Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa Bwana, Bwana akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema, 2. Musa mtu­mishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. 3. Kila mahali zita­kapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.(YOS 1:1-3)
Kitabu hiki kinaendeleza matukio ya vitabu vya Musa. Musa aliacha uongozi kwa Yoshua, aliye­wapeleka wana wa Israeli mpaka nchi ya ahadi. Matukio ya kitabu hiki 1408-1387 K.K.
Biblia ina mifano ya aina mbali mbali. Katika vitabu vya Musa mifano hiyo inatu­eleza namna ya kutoka katika utumwa wa Misri (yaani - kuokoka), tunavyovuka bahari ya Shamu (ni - ubatizo). Tunavyosafiri jangwani kuelekea nchi ya ahadi (maana yake - safari ya imani).
Mfano katika kitabu cha Yoshua ni tofauti. Inatueleza kuhusu kutekwa kwa nchi ya Kanaani. Ni mfano kwetu kwamba baada ya kuo­koka tuna­anza safari ya maisha ya rohoni na ahadi za Mungu zinavyotimizwa kwetu kadri tunavyozidi kusonga mbele.
KITABU CHA WAAMUZI
1. Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Isra­eli wakamwuliza Bwana, wakisema, Ni nani ata­kayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao? 2. Bwana akasema, Yuda ata­kwea; ta­zama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake. (AMU 1:1,2)
Kitabu cha Waamuzi kinaendeleza kitabu cha Yoshua. Jina la kitabu hiki kinatokana na kujazwa roho wale viongozi kumi na wawili, walio­itwa na Mungu kuwasaidia wana wa Israeli. Hekalu lilikuwa huko Silo, lakini watu wa­lipomkataa Mungu walishindwa kuka­taa kuingia kwa maadui. Mahakimu waliwakomboa kwanza Waisra­eli na baadaye wa­kaanza kazi zao za utawala. Walishughulika sehemu mbali mbali na sehemu zingine walitawala kwa pamoja.
Kitabu cha waamuzi kinaelezea kipindi cha giza ndani ya maisha ya Israeli katika nchi ya ahadi. Shindi zilizoko katika kitabu cha Yoshua ziligeuka hasara na uhuru ukawa utumwa na badala ya imani wakaanza kukosa imani. Kuendelea kukaanza kupungua wakapoteza macho ya kiroho na badala yake watu walianza kuwaza kiulimwengu.
Uaminifu kwa Mungu ukapungua badala ya furaha huzuni ikaingia, na badala ya nguvu kukaja unyonge. Umoja ukatoweka na kuzorota. Zamani dhambi ilihukumiwa lakini sasa dhambi ilikubaliwa. Watu walianza kumwacha Mungu naye aka­waacha mikononi mwa maadui. Israeli ilipoanguka lakini walipojuta na kumlilia Mungu yeye akawainulia ha­kimu aliyewakomboa. Kitabu kinaeleza kuhusu nyakati saba za ku­jiuzulu, nyakati saba za utumwa na saba za kuwekwa huru.
Matukio ya kitabu hiki yalifanyika 1387-1070 K.K. Matukio ya KI­TABU CHA WAAMUZI yalichukua zaidi ya miaka mia tatu. Matu­kio katika kitabu hiki hayako katika mpangilio wa miaka, kwani sura za mwisho zilifanyika kabla ya yale yaliyotangu­lia. Sura za nyuma zinaeleza jinsi anguko lilivyowapeleka wana wa Israeli mbali mapenzi ya Mungu.
Ujuzi wa Wayahudi wanafikiri nabii Samweli amekuwa mwandishi wa kitabu cha Waamuzi.
RUTHU
1. Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Aka­ondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili.(RUT 1:1)
Kitabu cha Ruthu ni kitabu cha mapenzi na ukombozi. Matukio yake yalitokea wakati wa kitabu cha Waamuzi. Mwandishi hajulikani lakini kwa sababu undugu unafika hadi wakati wa Daudi inawezekana kilia­ndikwa wakati wa utawala wa Daudi.
Kitabu kina mifano mingi. Wanaojulikana katika kitabu hiki ni Ruthu, mkwewe Naomi na atakayeendeleza ujamaa Boazi. Kwa mujibu wa Wayahudi inawezekana Samweli ameandika kitabu cha Ruthu.
VITABU VYA SAMWELI
Kitabu cha kwanza cha SAMWELI na kitabu cha pili cha SAMWELI.
1. Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Mwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri. (1SAM 3:1)
Katika vitabu vya Samweli kuna wahusika wakuu watatu: Samweli, Sauli na Daudi. Samweli alikuwa kiongozi wa mwisho wa­kati wa maha­kimu na pia nabii wa kwanza aliyejulikana. Sauli alikuwa mfalme wa kwanza Israeli na Daudi mfalme mkubwa na mpendwa zaidi.
Samweli alipopata wito, hali ya kiroho huko Israeli ilikuwa mbaya. Ukuhani wa kiroho ulikuwa umezorota, sanduku la agano limeibiwa lakini baa­daye likawa limerudishwa tena. Makuhani waliacha kazi zao na watu walikaa katika hali ya kusikitikia hasara yao. Anguko la watu lilisababisha wa wa­mwache Mungu kama mfalme na walitaka wanadamu badala yake kuwao­ngoza. Walimpata Sauli. Hivyo miaka mia tano ya utawala wa ki­falme ulianza Israeli.
Sauli pia alimwacha Mungu, ndipo Mungu alimwita Daudi badala yake. Wakati wa Daudi hali ya watu kiroho ilianza kuinuka tena. Ndani ya vitabu kuna maelezo mengi ya kihisto­ria na matukio lakini zaidi pia kuna mifano na mafundisho. Mwa­ndishi hajulikani labda Samweli ali­kusanya sehemu ya maelezo na walio­kuwepo wakati wa Daudi walikusanya baadhi.
Matukio yaliyofa­nyika wakati wa Kitabu cha kwanza cha Samweli mwaka wa 1115-1012 K.K. Matukio yalichukua miaka 103.
Kitabu cha pili cha Samweli kinaeleza wa­kati wa utawala wa mfalme Daudi, yaani 1012-972 K.K.
VITABU VYA WAFALME
Kuna vitabu viwili. Kitabu cha kwanza cha WAFALME na Kitabu cha pili cha WAFALME. Vitabu vya Wafalme ni endelezo ya vitabu vya Samweli. Kadri ya jina vitabu vinaeleza kuhusu uta­wala wa Daudi na Sulemani na wa­falme wa Yuda na Israeli. Utawala ulichukua kipindi cha miaka mia nne na inaeleza kukua na kuanguka kwa utawa­la.
Tunaona pia utawala ulivyogawanyika. Pia tunaona Yuda na Israeli walivyo pe­lekwa uhamishoni. Utawala wa kusini, yaani Yuda, ulikuwa na wafalme ishirini na utawala wa kaska­zini, yaani Israeli, walikuwepo kumi na tisa. Uhamisho ulitokana na kutokutii. Elisha na Eliya pia wanapatikana kama manabii wenye nguvu.
Wayahudi wanamfahamu nabii Yeremia kama mwandishi wa vitabu hivi. Wakati wa Kitabu cha kwanza cha WA­FALME ni 972-853 K.K. Wakati ulichukua kama miaka 119. Muda wa Kitabu cha pili cha WAFALME: 853-562 K.K. Ilichukua muda kama miaka 291. Jumla ya miaka Vitabu vya WAFALME ni miaka 410. Kumbuka: Siyo kamili.
8. Hata mwezi wa tano, siku ya saba ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na kenda wa mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Ye­rusalemu. 9. Akaiteketeza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto. 10. Na jeshi lote la Wakalda­yo, waliokuwa pamoja na huyo amiri wa askari walinzi, wakazibomoa kuta za Yerusalemu pande zote. (1FAL 25:8-10)
Vitabu vya WAFALME vinaanza kwa ujenzi wa hekalu na kunamali­zika kwa kuchomwa kwake.
Kitabu cha kwanza cha MAMBO YA NYAKATI.
Sura za mwanzo wa MAMBO YA NYAKATI ni elimu ya ukoo. Ni vizuri tuyachunguze. Roho Mtakatifu atakapotufunulia elimu ya ukoo, tutapata hazina nyingi. Sura hizi zinatueleza kwamba Yesu ni mrithi wa kiti cha utawala wa Daudi. Elimu ya ukoo pia inatueleza watu wali­potokea. Wayahudi wanathamini sana sura hizo kwa sababu wanamsu­biri Masihi wao. Tunajua: Yesu ni Masihi. Lakini bado Wayahudi ha­waamini Yesu ni Masihi.
Kitabu kinatueleza kuhusu Daudi vivyo hivyo kama Kitabu cha pili cha SAMWELI kinavyotueleza. Elimu ya ukoo inaanzia Adamu, lakini matukio yanaanza mwaka wa 1012 K.K. Ma­tukio katika Kitabu cha kwanza cha MAMBO YA NYAKATI yana­endelea hadi mwaka wa 972 K.K. Mwandishi wa kitabu hatuna uhaki­ka, lakini inafikiriwa kwamba kuhani Esra ndie aliyekiandika.
Kitabu cha pili cha MAMBO YA NYAKATI.
Kitabu hiki kinaendeleza mambo ya Nyakati wa Kwanza. Kitabu kina­anza na utawala wa Sule­mani na kueleza zaidi kuhusu Israeli ya kusini yaani wafalme wa Yuda. Historia yao kwa sehemu kubwa ni jinsi wali­vyoanguka na baada ya yote hekalu liliteketezwa hata watu wakapele­kwa uhamishoni Babeli. Hekalu lilikuwa limetumika miaka 375 na liliteke­tezwa mwaka wa 586 K.K.
Danieli na Ezekieli walikuwa miongoni mwa wale waliohamishwa kwa nguvu Babeli. Kitabu kinamalizika kwa Wayahudi ku­pewa ruhusa na Koresi kurudi nchini kwao. Kitabu kinaanza kwa matukio ya mwaka wa 972 na kumalizika kwa ma­tukio ya mwaka wa 538 K.K.
EZRA
1. Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kuti­mizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uaje­mi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema. (EZR 1:1)
Kitabu hiki kina sehemu mbili. Sura ya kwanza hadi sita zinaelezea kujengwa tena kwa hekalu. Sura ya saba hadi kumi kufufuliwa kwa ibada za Mungu. Kati ya sura ya kwanza hadi sita na saba hadi kumi kuna miaka sitini. Wakati huo matukio ya kitabu cha ESTA yalitokea.
Katika sura za mwanzo tunaelezwa jinsi wale waliopelekwa uhamishoni walivyorudi Israeli. Ni elfu hamsini tu walirudi. Wengi wali­baki Babeli. Waliorudi walianza tena kujenga hekalu. Baadaye wali­pomaliza msingi waliacha kazi hiyo kati kati bila kukamilika. Wali­choshwa na upinga­mizi pamoja na ukubwa wa kazi.
Baada ya miaka kumi na sita Mungu aliwaita wanaume wawili Hagai na Zekaria walio­ongea wazi wazi juu ya mwenendo wa watu na wakakazia kutokujali kwao mambo ya Mungu. Matokeo ya shughuli za manabii hawa wawili watu walitiwa moyo wa kuendelea na kazi ya kujenga hekalu tena. Hekalu likawa tayari miaka ishirini baada ya waliopelekwa uhamishoni kurudi. Hivyo hekalu lili­kuwa gofu kwa miaka sabini.
Ezra aliingia Yerusalemu miaka sitini baadaye. Alikuja kuinua maisha ya watu kiroho yaliyokuwa katika hali mbaya. Kuta zilikaa bila kuje­ngwa na Wayahudi walikuwepo chini ya maangamizi makubwa. Baada­ye Nehemia alikuja kujenga kuta na mji.
Matukio: 538 K.K. Wayahudi kama 50.000 wali­rudi Yerusa­lemu kufuatia wito wa Zerubabeli. (2NYA 36:22,23). Baada ya mwaka mmoja msingi wa He­kalu ulijengwa. Lakini baadaye kazi ilisimami­shwa. Mwaka wa 520 ujenzi wa Hekalu ulianza tena. Manabii walikuwa Hagai na Ze­karia. Mwaka wa 516 kabla ya Kristo Zerubabeli alifungua Hekalu. Mwaka wa 457 kabla ya Kristo Ezra aliingia Yerusa­lemu pamo­ja na Wayahudi elfu mbili.
NEHEMIA
1. Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisleu, mwaka wa ishirini, nilipo­kuwapo Shushani ngomeni, (NEH 1:1)
Mungu alimwita Nehemia mwaka wa 445 kabla ya Kristo, miaka kumi na minne baada ya kurudi kwa Ezra. Wa­zazi wa Nehemia walikuwa hawaja­ondoka bado, wakati Wayahudi wali­popata uhuru kutoka uha­mishoni. Mfalme alikuwa ni Artashasta. Yeye alikuwa kijana wa tatu wa mume wake Esta Ahasuero.
Artashasta ali­wapenda Wayahudi. Inawe­zekana alifanya hivyo kwa ajili ya Esta, mama yake wa kambo. Nehe­mia alikuja kujenga mji wa Yeru­salemu na kuta zake. Nehemia alipofi­ka, Hekalu lilikuwa limekamilika miaka sabini. Katika sura za mwisho za Kitabu cha NEHEMIA zinaele­za Nehemia ali­tengeneza maisha ya watu kiroho. Matukio ya kitabu hiki yalifanyika 445-432 K.K.
ESTA
1. Zamani za Ahasuero; naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na ishirini na saba; (EST 1:1)
Kitabu cha ESTA ni cha ajabu sana katika Biblia. Ndani yake Mungu hatajwi, hakuna neno linalogusia mambo ya rohoni. Hata hivyo kitabu hiki kina ujumbe mzuri wa kiroho: Kanisa la Mungu limechukuliwa badala ya Wayahudi.
Mwandishi hajulikani. Matukio yalitokea wakati wa Kitabu cha EZRA. Yaani mwaka wa 486-465 K.K. Esta alibaki mjane akiwa na umri chini ya miaka arobaini alikuwa ameolewa na Ahasuero kwa muda wa miaka kumi na minne.
AYUBU
1. Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake ali­kuwa akiitwa Ayu­bu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kue­pukana na uovu. (AYU 1:1)
Kitabu kinajadili: Kwanini watakatifu wanateseka.
Marafiki zake Ayubu watatu wana­mlaumu Ayubu kwamba anateseka kwa ajili ya dhambi zake. Ayubu alielewa mambo hayo tofauti. Sura ya mwisho Mungu anasema kwamba marafiki zake Ayubu wali­ongea vibaya.
Kitabu hiki kimewafariji wengi katika matatizo yao. Inawezekana mambo haya yalitokea wa­kati wa Ibrahimu. Mwandishi hajulikani, wengine wanafi­kiri kwamba ni Musa aliyeandika Kitabu cha AYUBU. Kitabu hiki ni cha zamani zaidi ndani ya Biblia.
ZABURI
1. Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; wala hakusi­mama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. (ZAB 1:1)
Jina la Zaburi kwa Kiebrania ni Sefer tehillim, maana yake ni nyimbo za sifa. Kitabu hiki msingi wake ni sifa, ibada, kukiri dhambi na mao­mbi. Kitabu hiki ni kitabu cha maombi ya Wayahudi na Wakristo pia. Ujumbe ndani ya ZABURI unahusu ma­gumu na ushindi wa watu wa Mungu na kupingana na magumu katika hali mbali mbali. Pia ZABU­RI zina ufunuo mwingi.
Waandishi: Daudi aliandika Zaburi sabini na tatu, Asafu kumi na mbili, Wakorohi kumi na mbili, Sulemani mbili, Musa moja, Etani moja na bila majina ya walio­ziandika ni arobaini na tisa.
Wakati wa kuziandika: Musa aliandika kama mwaka wa 1450 K.K. Daudi alikuwa mfalme tangu mwaka wa 1012-972 K.K. Na aliandika Zaburi sabini na tatu. Zaburi chache ziliandikwa huko Babeli wakati wa uhamisho, nyingine baa­daye. Uhamisho ulimalizika mwaka wa 539 kabla ya Kristo. Na hivi ZABURI ziliandikwa kwa muda wa miaka elfu moja hivi.
MITHALI
Mithali ni vitabu vya maarifa ya Masha­riki ya kati. Kwa nini MITHA­LI iko katika Biblia?
1. Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli. 2. Kujua hekima na adabu; kutambua ma­neno ya ufahamu; 3. kufundishwa matendo ya bu­sara, katika haki na hukumu na adili. 4. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; 5. mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufa­hamu ayafikie mashauri yenye njia. (MIT 1:1-5)
Zaidi sana ni kwa vijana inaeleza ku­husu mambo ya rohoni, na tabia njema inayolenga mambo juu ya maisha ya furaha duniani, na zawadi katika maisha yajayo. Kitabu kina ujumbe wa mifano.
Waandishi: Sulemani, Aguri na Lemueli. Muda: Sulemani alikuwa mfalme mwaka wa 972-932 K.K. Aguri na Lemueli hawajulikani. Hatujui, waliishi lini.
MHUBIRI
1. Maneno ya Mhubiri, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu 2. Mhu­biri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubati­li. (MHU 1:1,2)
Kitabu hiki kinatofautiana na vitabu vi­ngine ndani ya Biblia. Kitabu hiki kinaweza kumchanganya msomaji kwa sababu kinakubali mambo machache ambayo hayakuba­liwi ndani ya Biblia. Ndani yake kuna kukata tamaa na kuchoka.
Matatizo haya yataisha tutakapoelewa kwamba Sulemani alipokuwa katika mwisho wa maisha yake na katika hali ya kuanguka aliandika kitabu hiki. Sulemani alipoanza katika kuabudu miungu mingine moyo wake ulita­futa faraja kutoka katika vitu mbali mbali na hapa anatueleza kuhusu kutafuta kwake. Hakupata.
13. Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha si­kiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. (MHU 12:13)
Hivyo hatutembei katika njia zile alizo­tembea Sulemani wakati wa ma­anguko yake.
WIMBO ULIO BORA
Kitabu hiki kina mifano mingi:
  • Upendo wa Mungu juu ya Israeli.
  • Upendo wa Kristo kwa kanisa.
  • Na upendo kati ya bwana arusi na bibi arusi.
Pia kitabu kinatueleza juu ya upendo safi wakati wa ndoa. Inawezekana ni Sulemani aliyekiandika. Kitabu hiki ni kizuri zaidi duniani cha mapenzi. Sulemani alitawala mwaka wa 972-932 K.K. Wakati huo aliandika kwanza WIMBO ULIO BORA, na baadaye MHUBIRI.
ISAYA
1. Haya ni maono ya Isaya, mwana wa Amozi, aliyo­yaona katika habari za Yuda na Yerusalemu, siku za Uzia na Yothamu na Ahazi na Heze­kia, wafalme wa Yuda. (ISA 1:1)
Isaya anaanza katika mlolongo wa ma­nabii wa Biblia. Yeye aliishi mwaka wa 750-680 kabla ya Kristo. Watu wachache wanafikiri kuwa kitabu cha Isaya hakikuandikwa na mtu mmoja labda wawili au watatu. Biblia haijibu swala hili na pia siyo muhimu sana. Lakini kitabu kina­eleza kwamba Isaya ameandika kitabu kizima.
Isaya aliionya Israeli ya ka­skazini ku­husu dhambi lakini hawakujali ma­onyo. Katika kitabu cha Isaya sehemu ya mwisho ni ya faraja kwa Israeli ya kaskazini watakao­pelekwa uhami­shoni Ashuru kwenye mwaka wa 722 K.K.
Kitabu cha Isaya kinamzungumzia Ma­sihi zaidi. Kina ufunuo juu ya Masihi zaidi kuliko vitabu vingine vya manabii. Wafalme wakati wa Isaya walikuwa ni Uzia, Yothamu, Ahazi, Hezekia na Manase. Isaya anatangaza hukumu tangu sura ya kwanza hadi ya thelathini na tisa. Na anatangaza faraja kwanzia sura ya arobaini hadi sitini na sita.
YEREMIA
1. Maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani walio­kuwa katika Anathothi, katika nchi ya Benyamini; (YER 1:1)
Isaya aliishi wakati wa utawala wa Ashuru, na Yeremia aliishi wakati wa utawala huo ulipokuwa ume­anguka tayari. Na Babeli na Misri wanago­mbana ili kutwaa utawala wa dunia nzima na Babeli ilishinda. Yeremia aliionya Yuda yaani Israeli ya kusini kuhusu dhambi lakini hawa­kujali maonyo. Hivyo anguko liliwakuta Yuda pia. Babeli iliangamiza Yuda, yaani Israeli ya kusini.
Katika kitabu cha YEREMIA matukio hayana mpangilio maalum. Mahubiri mengi ya Yeremia yalipati­kana wakati wa utawala wa Yeho­ya­kimu na Sedekia. Yeremia alishughulika mwaka wa 627-586 K.K.
MAOMBOLEZO
Israeli alipokuwa akipelekwa uhami­shoni na Yerusalemu tayari ime­angamizwa Yeremia alianza ku­andika kitabu cha Maombolezo kwa machozi. Hayo yalitokea baada ya kubomolewa kwa hekalu mwaka wa 586 kabla ya Kristo. Kitabu kimeandikwa mfano wa shairi. Yeremia alilia Yerusalemu kama ali­vyofanya Kristo miaka mia sita baa­daye.
1. Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi ali­vyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya ma­jimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa! (OMB 1:1)
EZEKIELI
1. Ikawa katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa pamoja na watu waliohamishwa, karibu na mto Kebari, mbingu zi­lifunuka, nikaona maono ya Mungu. (EZE 1:1)
Ezekieli alipelekwa Babeli mwaka wa 597 kabla ya Kristo. Baada ya miaka mitano alianza kutoa unabii. Mke wa Ezekieli alifariki siku ile ile jeshi la Babeli lilipoanza kuzunguka mji wa Yerusalemu, mwaka wa 588 kabla ya Kristo. Ezekieli aliendelea kutoa unabii hadi mwaka wa 570 au zaidi kidogo.
Yeye alikuwa mtumwa vijijini bali Da­nieli mjini Babeli. Ezekieli alitoa unabii juu ya Yerusalemu na mataifa mengi. Pia alitoa unabii juu ya siku zijazo juu ya Israeli mazuri. Sehemu kubwa ya utabiri wake ilikwi­shatokea, lakini bado sehemu ndogo tu.
DANIELI
1. Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehoya­kimu, mfalme wa Yuda, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alikwenda Yerusalemu akauhusuru. 2. Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ka­tika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akavi­ingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake. (DAN 1:2)
Kitabu cha Danieli kiliandikwa wakati wa uhamisho wa Babeli. Ukoo wa Danieli ulikuwa wa kifalme na hivyo alikuwa wakwanza kupe­lekwa uhamishoni mwaka wa 605 kabla ya Kristo. Alishughulika Babeli kwa muda mrefu. Aliendelea hadi mwaka wa 530 kabla ya Kristo.
Wakati wa Danieli walikuwepo pia Ye­remia na Ezekieli. Yeremia ali­hubiri Israeli, na Ezekieli katika vijiji vya Babeli na Danieli katika mji wa Babeli. Danieli alipokuwa amekaa Babeli karibu miaka ishirini hekalu la Yerusalemu lilibomolewa. Ilitokea mwaka wa 586 kabla ya Kristo na wakati huo Wayahudi wengi walipelekwa Babeli.
Kitabu cha Danieli kina unabii mwingi tofauti. Mengine yalitokea kabla ya Kristo, mengine bado hayajatimia.
HOSEA
1. Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Hosea, mwana wa Beeri, siku za Uzia, na Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli. (HOS 1:1)
Hosea aliishi na kutoa unabii huko Israeli ya kaskazini. Yeye alisikia matatizo makubwa juu ya watu wake. Katika kitabu chake anaelezea juu ya kumwacha mke asiyemwaminifu. Ni mfano wa Israeli. Na pia anae­leza Israeli itarudi kwa Mungu baadaye. Ingawa kitabu kina hukumu lakini pia tunasoma kuhusu upendo wa Mungu juu ya watu wake.
Hosea aliishi mwaka wa 770-700 kabla ya Kristo.
YOELI
1. Neno la Bwana lililomjia Yoeli, mwana wa Pethu­eli. 2. Sikieni haya, enyi wazee; Sikilizeni, enyi we­nyeji wote wa nchi. Je! mambo haya yamekuwako katika siku zenu, Au katika siku za baba zenu? (YOE 1:1,2)
Inaonekana Yoeli aliishi kati ya mwaka wa 800 na 700 kabla ya Kristo. Lakini hatujui kamili. Yeye alitabiri juu ya fumbo la panzi, siku ya Bwana na matukio yake. Yeye alitabiri juu ya siku ambazo hazija­fika bado. Yeye ni nabii aliyeangalia mbali ku­pita hata wakati wetu. Aliona pia Roho Mtakatifu atafika duni­ani. Na ilito­kea katika sikukuu ya Pente­koste.
AMOSI
1. Maneno ya Amosi, aliyekuwa mmoja wa wachu­ngaji wa Tekoa; mao­no aliyoyaona katika habari za Israeli, siku za Uzia, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Isra­eli, miaka miwili kabla ya tete­meko la nchi. (AMO 1:1)
Amosi alikuwa mchunga mifugo aliye­lima mizabibu mwitu. Alitabiri vikali juu ya ubaya wa Israeli. Hali ya watu kiroho ilikuwa mbaya la­kini kimwili ilikuwa nzuri. Amosi alitumika mwaka wa 765-750 kabla ya Kristo. Wafalme wakati huo walikuwa: Yerobo­amu wa pili katika Israeli ya kaska­zini na Asaria, yaani Uzia, Israeli ya kusini, yaani Yudea. Aliwakemea watu wa Israeli walioishi katika dhambi.
OBADIA
1. Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana Mungu juu ya Edomu; Tu­mepata habari kwa Bwana, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Haya, inukeni ninyi; Na tuinuke tupigane naye. (OBA 1:1)
Kitabu hiki ni kifupi zaidi ndani ya Agano la Kale. Inawezekana Oba­dia aliishi na kutu­mika kati ya mwaka wa 800 na 600 kabla ya Kristo. Hatujui kamili. Yeye alitangaza hukumu juu ya Edomu, yaani kwa uzao wa Esau, kwani wao waliwasumbua watu huko Yudea kwa fujo zao.
YONA
1. Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Ami­tai, kusema, 2. Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu. (YON 1:1,2)
Yona aliishi kati ya mwaka wa 700 na 600 kabla ya Kristo. Anajuli­kana kwa kukaa ndani ya tumbo la samaki. Labda alikuwa amekufa tumboni mwa samaki. Baada ya samaki ku­mtapika alifufuka. Kwa kadri ya Wayahudi inawezekana Yona alikuwa kijana wa mjane wa Sa­repta aliyefufuliwa na Eliya. (1FAL 17:17-22). Yona anajulikana kama mmi­sionari wa wapagani na kwa sababu ya mahu­biri yake watu wa Ninawi walimge­ukia Mungu.
MIKA
1. Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Mika, Mmo­rashu, katika siku za Yotha­mu, na Ahazi, na Heze­kia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona katika habari za Samaria, na Yerusalemu. (MIK 1:1)
Mika alitumika pamoja na Isaya, yaani yeye aliishi mwaka wa 750-680 kabla ya Kristo. Mika aliwahubiria watu wa kawaida wa Samaria na Yerusalemu. Alizungumza juu ya hukumu ijayo, uta­wala wa Masihi na neema ya mwisho kwa Waisraeli.
NAHUMU
1. Ufunuo juu ya Ninawi. Kitabu cha maono aliyoya­ona Nahumu, Mwelkoshi. (NAH 1:1)
Nahumu alitumika wakati wa mfalme Yosia, yaani mwaka wa 640-609 kabla ya Kristo. Yeye alitabiri maangamizi ya Ninawi. Ninawi ilikuwa mji mkuu wa Ashuru zamani. Umoja wa jeshi la Wamedi na Babeli uliangamiza Ninawi, ilitokea mwaka wa 612 kabla ya Kristo. Nabii Yona alikuwa ametabiri, kwamba Ninawi itaangamizwa. Ufunuo wa Yona ulitokea miaka mia mbili baadaye.
HABAKUKI
1. Ufunuo aliouona nabii Habakuki. (HAB 1:1)
Habakuki ni nabii asiyejulikana na ali­fanya kazi pamoja na nabii Na­humu. Yeye anaingia kutatua swala kubwa la kiteolojia, yaani elimu ya dini: Inawe­zekanaje kuweka pamoja: utakatifu wa Mungu na ustahimi­livu wake wa­kati wa kuhukumu mabaya. Na aliuliza: kwa nini Mungu anajali wa­baya wanaoendelea kufanya mambo mabaya?
SEFANIA
1. Neno la Bwana lililomjia Sefania, mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia; katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda. (SEF 1:1)
Sefania alitumika mwaka wa 638-608 kabla ya Kristo. Alikuwepo wakati wa Yeremia na ali­kuwa sababu ya uamsho uliofanyika wakati wa Yosia. Aliongea juu ya hukumu ya Yudea na makabila mengine na kuhusu Israeli itakavyostawi wakati wa utawala wa Masihi.
HAGAI
1. Katika mwaka wa pili wa Dario mfalme, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana lili­mjia Zerubabeli, mwana wa Shea­ltieli, liwali wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake Hagai nabii, kusema. (HAG 1:1)
Tumesoma: Katika mwaka wa pili wa Dario mfalme. Ni sawa sawa mwaka wa 520 kabla ya Kristo. Waisraeli waliorudi Babuloni wali­kuwa wameanza kujenga hekalu la­kini waliacha kujenga kwa sababu ya upi­ngamizi. Baada ya kuhimizwa na Hagai na Ze­karia walianza kujenga hekalu tena hadi likakamilika.
ZEKARIA
1. Katika mwezi wa nane, mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria, mwana wa Bere­kia, mwana wa Ido, nabii, kusema, (ZEK 1:1)
Tumesoma: ... mwaka wa pili wa Dario. Ndiyo, ilifanyika mwaka wa 520 kabla ya Kristo. Zekaria aliona maono maku­bwa, zaidi kuhusu Masihi na wakati wake. Sura za mwisho zinaeleza kuhusu yata­kayoto­kea baadaye. Kuhusu kuja kwa Kristo na mambo ya­nayohusu hayo. Kitabu cha Zekaria kinatangaza wazi wazi yatakayoto­kea wakati wa mwisho.
MALAKI
1. Ufunuo wa neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki. (MAL 1:1)
Malaki ni nabii wa mwisho katika Agano la Kale. Aliishi karne ya nne kabla ya Kristo. Yeye alitabiri juu ya atayekuja kabla ya Masihi, yaani Yohana mbatizaji. Malaki aliona mbali na aliona siku ya Bwana yaani ghadhabu ambapo Israeli itakombolewa.
Kati ya Agano la Kale na Agano Jipya
Wakati huo ni miaka kama mia nne.
Mwanzoni Uajemi ilitawala dunia nzima hadi hapo mwaka wa mia tatu Ugi­riki ilipojiimarisha. Kama mwaka wa mia moja kabla ya Kristo Wayahudi walilazimishwa wawe Wagiriki kwa lazima.
Wayahudi walipambana kwa hali tofauti tofauti.
Septuaginta ilitayarishwa mwaka wa mia moja na hamsini Kabla ya Kristo.
Septuaginta ni tafsiri ya zamani ya Agano la Kale iliyoandikwa kwa lugha ya Kigiriki. Rumi iliimarika pole pole na maeneo ya Israeli yaani Palestina yaliingia chini ya utawala wa Rumi mwaka wa 63 kabla ya Kristo.
Na hivi tumechunguza tayari Agano la Kale kwa ufupi.
Agano Jipya
Agano Jipya ni mkusanyo wa vitabu ishi­rini na saba. Vitabu hivi vilia­ndaliwa na watu mbali­mbali. Vitabu vya Agano Jipya viliandikwa mnamo kati ya mwaka wa hamsini na wa tisini na tano baada ya Kristo. Vitabu vinatofautiana kwa namna mba­limbali. Lakini vyote vinahusu jambo hili moja kwamba Yesu Kristo aliwajia watu, akawa­onyesha kwamba yeye ndiye mwenye kuwapa uhai na uhuru wa kweli. Na pia yeye huwafanya watu wawe we­nyeji wa ufalme wake, ufalme wa haki, upendo na amani. Kwa waandishi hao, jambo hili la Mungu ku­wajia watu wake katika nafsi yake Yesu Kristo ndilo Injili, yaani Habari Njema.
Agano Jipya laanzia na Injili nne. Hivi ni vitabu ambavyo vinatupatia ha­bari juu ya matendo na mafundisho ya Yesu. Na kwamba alikufa msalabani kwa ajili yetu na juu ya ufufuo wake ambao kwa huo ameshinda nguvu za kifo. Injili tatu za kwanza: MATHAYO, MARKO na LUKA zinafanana sana kuhusu mambo muhimu yaliyomo. Injili ya nne, yaani ile iliyoandikwa na YOHANA, ina mpango mwingine tofauti na huo unaofuatwa na Injili hizo za Mathayo, Marko na Luka.
Hata hivyo, waandishi wote wanne wana­andika kwa lengo moja: Habari Njema ya wokovu aliotuletea Bwana wetu Yesu Kristo. Kila Injili basi inayo nafasi yake muhimu katika kutuelewesha Yesu Kristo ni nani katika maisha yetu kwa kutujulisha juu ya matendo, mafundisho, kifo na ufufuo wake, matukio ambayo yana­husu kukombolewa kwa bina­damu ku­toka katika nguvu za dhambi na kifo.
Katika kitabu cha MATENDO YA MITUME, tunaambiwa juu ya kuenea kwa Habari Njema, kuanzia Yerusalemu mpaka Rumi. Baada ya kitabu hicho zinafuata barua kumi na tatu za Paulo. Mtume Paulo alisafiri sana akihubiri Habari Njema kokote alikokwenda. Katika safari zake hizo aliwahi kuanzisha jumuiya nyingi za Kikristo. Akiwa mbali na jumuiya hizo alitaka kuonana nazo walau kwa barua. Aliandika agha­labu kutatua matatizo ya­liyozuka katika jumuiya. Baadhi yake yakiwa yamesababishwa na wapinzani wake. Pia aliandika kwa shabaha ya kuwaima­risha viongozi wa jumuiya hizo.
Baada ya barua za Paulo, tunayo barua kwa WAEBRANIA. Lengo la barua kwa Waebrania ni kue­leza waziwazi uhusiano kati ya Yesu Kristo na Agano la Kale. Barua nyingine saba zinazofuata baada ya barua kwa Waebrania haziku­andikwa kwa jumuiya fulani, bali za­husu matatizo yanayowakumba Wa­kristo wote na imani yao wanapoishi katika dunia hii. Mwisho kabisa tunacho kitabu cha pekee kijulikanacho kama kita­bu cha UFUNUO. Kitabu hiki kinahusu mambo ya mwisho, nyakati ambapo Mungu atakamilisha ufalme wake. Na mwishowe Mungu ata­tawala milele.
Vitabu vya Agano Jipya tunaweza kuvi­panga hivi: Injili – vitabu vinne – MATHAYO, MARKO, LUKA na YOHANA. Historia – kitabu kimoja – MATENDO YA MITUME. Unabii – kimoja – UFUNUO. Nyaraka ishirini na moja. Paulo aliandika nyaraka kumi na tatu, we­ngine saba. Hatujui, ni nani aliandika waraka wa WAEBRANIA.
Katika Biblia kuna sura 1.189. Katika Agano la Kale kuna sura 929. Na Agano Jipya 260. Katika Biblia ya kiswahili kuna mistari 31.102. Ambazo ni katika Agano la Kale mistari 23.145. Na mistari 7.957 katika Agano Jipya.
MATHAYO
1. Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. 2. Ibrahimu aliamzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo aka­mzaa Yuda na ndugu zake; (MT 1:1,2)
Mwandishi ni Myahudi wa Galilaya mtoza ushuru kwa jina aliitwa Ma­thayo, yaani Lawi. Yeye alikuwa katika kundi la wanafunzi wa Yesu wa karibu zaidi. Kitabu kiliandikwa mwaka wa hamsini baada ya Kristo. Mathayo aliwaandikia Wayahudi kwamba Yesu Kristo akiwa ni mfalme wa Israeli.
Kwa sababu aliwaandikia barua yake Wayahudi, Wayahudi wanaelewa Injili ya Mathayo vizuri. Mathayo alipoanza barua yake, kwanza aliandika orodha ya ukoo wa Yesu. Hivi aliwao­nyesha, kwamba Yesu ni mwana wa Daudi, yaani Yesu ni Ma­sihi.
19. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wana­funzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20. na kuwafundisha kuya­shika yote ni­liyowaamuru ninyi; na ta­zama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. (MT 28:19,20)
MARKO
1. Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. (MR 1:1)
Inawezekana Marko alikuwa sawasawa na Yohana Marko, kijana wa Mariamu. Yeye aliondoka pamoja na Barnaba na Paulo kwa kazi ya misheni, lakini ali­rudi muda mfupi baadaye.
Marko aliandika kati ya mwaka wa sitini na nne, na sitini na nane. Aliwaandikia Warumi na kueleza kwamba Kristo ni mwana wa Mungu. Wakati huo Warumi walitawala Israeli na karibu dunia nzima. Walielewa vizuri Marko alipowaandikia barua yake.
20. Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana aki­tenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo. (MK 16:20)
LUKA
1. Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, 2. kama walivyotuhadithia wale wa­liokuwa masha­hidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3. nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nime­jitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu, 4. upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa. (LK 1:1-4)
Mwandishi ni daktari Luka. Yeye aliwaandikia Wagiriki namna gani Yesu ni mtoto wa mwanadamu. Wagiriki walimwelewa Luka vizuri. Luka aliwahoji waliokuwepo na kuwa­uliza maoni yao.
Yeye hakueleza mambo kwa mpangilio, bali alieleza jinsi alivyoelezwa na mtu mmoja kwanza, halafu akaeleza ya mwingine. Inawezekana aliandika huko Kaisaria wakati Paulo alipokuwa amefungwa mwaka wa hamsini na nane baada ya Kristo.
50. Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. 51. Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. 52. Wa­kamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu. 53. Nao wa­likuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu. (LK 24:50-53)
YOHANA
1. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.(YN 1:1)
Kazi ya Yohana zamani ilikuwa uvuvi, kama ndugu yake Yakobo. Wao waliitwa wana wa Ngurumo. Yohana alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu. Alikuwa karibu na Yesu na alimpenda Yesu sana.
Yeye aliandika kwamba Yesu ni Mungu. Injili ya Yohana ni rahisi zaidi kuielewa kwani yeye aliwaandikia watu wote. Watu wanaotaka kuokoka, wana­elewa zaidi Injili ya Yohana. Barua aliyoandika ni rahisi kuielewa. Haijulika­ni iliandikwa muda gani.
30. Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. 31. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. (YN 20:30,31)
Injili ya Yohana imeandikwa ili mpate kua­mini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Kwa ajili ya hii watu wengi wameokoka, kwa sababu Yohana alia­ndika Injili yake kwa wengi ili waweze kumwamini Yesu.
MATENDO YA MITUME
1. Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Teofilo, katika ha­bari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufu­ndisha, (MDO 1:1)
Luka aliandika Matendo ya Mitume pia. Inawezekana kiliandikwa labda mwaka wa sitini na tatu. Kitabu kinatuleza kuja kwa Roho Mta­katifu duniani, kuenea kwa Ukristo na matatizo ya mwanzoni. Wakati mwingine Luka alitembea pamoja na Paulo na kueleza juu ya mambo ali­yoyaona kwa macho. Kitabu hakina mwisho maana Matendo ya Mitume yanaendelea hata sasa.
WARUMI
1. Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu; ..... 16:27. Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina. (RUM 1:1, 16:27)
Paulo aliandika barua nyingi. Katika Biblia kuna barua zake kumi na tatu. Barua kwa WARUMI ni ya sita ya Paulo. Aliandika barua hii akiwa Korintho wa­kati wa safari yake ya tatu ya misheni. Aliiandika mwaka wa hamsini na saba au hamsini na nane. Alikuwa na katibu wake Tertio. (RUM 16:22).
Kwenye kitabu hiki anaongelea dhambi na haki na pia ahadi alizopewa Israeli na namna gani Wakristo wanaweza kue­nenda katika imani.
WAKORINTHO WA KWANZA
1. Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa ma­penzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, ..... 16:24. Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu. (2KOR 1:1, 16:24)
Kitabu cha nne cha Paulo kwa makanisa. Iliandikwa kutoka Efeso mwaka wa hamsini na nne au hamsini na tano. Matendo ya Mitume sura ya kumi na tisa inaeleza mambo yalitokea wakati huo. Paulo ali­tuma barua hii kupitia kwa Ste­fana, Fortunato na Akaiko. (1KOR 16:17).
Wakorintho walikuwa wachanga kiroho na wenye tabia ya mwi­lini. Barua ya Paulo pamoja na karama za Roho ziliwasaidia kurekebi­sha mambo pole pole.
WAKORINTHO WA PILI
1. Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu; kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walio­ko katika nchi yote ya Akaya. 2. Neema na iwe kwenu na amani, zito­kazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. (2KOR 1:1,2)
Barua ya tano ya Paulo. Iliandikwa mwaka wa hamsini na saba. Paulo anatetea kazi yake. Wakorintho walikuwa wameanza kukua kiroho baada ya kupata barua ya kwanza.
14. Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. (2KOR 13:13).
WAGALATIA
6. Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliye­waita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. (GAL 1:6)
Barua ya tatu ya Paulo. Iliandikwa mwaka wa hamsini na tatu. Hapa Paulo anatetea Injili ya neema kwa sababu wahubiri wa sheria waliku­wa wameharibu kazi ya Mungu kanisani huko Galatia. Pia Paulo anake­mea watu wa Galatia, wa­lipoiacha Injili ya neema.
1. Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? (GAL 3:1)
WAEFESO
1. Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; (EFE 2:1)
Barua ya saba ya Paulo. Iliandikwa kutoka gerezani huko Rumi mwaka wa sitini na moja au sitini na mbili. Barua inaeleza kuhusu maisha ya kanisa na siri ya kanisa.
32. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. (EFE 5:32)
WAFILIPI
3. Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, (FIL 1:3)
Barua ya kumi ya Paulo. Iliandikwa kutoka kifungoni Rumi kwenye mwaka wa sitini na mbili. Ujumbe wa barua hii ni unahusu zaidi nia ya Kikristo na jinsi ya kutosheka Kikristo katika hali mbali mbali. Kitabu kinaonyesha kwamba tunaweza kufurahi wakati wa mapungufu, mata­tizo na hata mateso.
5. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; (FIL 2:5)
WAKOLOSAI
1. Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu, ... 4:18. Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Ku­mbukeni ku­fungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi. (KOL 1:1, 4:18)
Barua ya nane ya Paulo. Aliiandika akiwa kifungoni huko Rumi mwaka wa sitini na mbili. Paulo alikuwa hajaenda Kolosai. Yeye aliku­wa na wasi wasi juu ya mafu­ndisho ya pembeni yaliyotaka kuingia kanisani. Ndio maana alimtuma Epafra huko Ko­losai pamoja na barua kwa kanisa. Katika barua hapa anajaribu kuinua uta­katifu wa Kristo.
WATHESALONIKE WA KWANZA
2. Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu. 3. Wala hatuachi kuiku­mbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu. ... 7. Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waa­minio katika Makedonia, na katika Akaya. 8. Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote. (1THE 1:2,3,7,8)
Barua ya kwanza ya Paulo kwa maka­nisa. Iliandikwa kutoka Korintho mwaka wa hamsini. Kanisa la Thesalonike lilikuwa mfano mzuri kwa makanisa mengine. Paulo alitaka kulitia moyo kanisa changa na pia kueleza mambo ya nyakati za mwisho.
5:28. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. (1THE 5:28)
WATHESALONIKE WA PILI
1. Paulo, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathe­salonike, lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo. (2THE 1:1)
Barua ya pili ya Paulo kwa makanisa. Iliandikwa kutoka Korintho mwaka wa hamsini na mbili. Kanisa liliishi katikati ya mateso na wa­lifikiri wameingia kwenye ghadhabu. Paulo aliwatolea wasi wasi wao na ali­taka kuhimiza kanisa liweze kuendelea mbele.
3:18. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. (2THE 3:18)
TIMOTHEO WA KWANZA
1. Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu, taraja letu; 2. kwa Ti­motheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. (1TIM 1:1,2)
Barua ya kumi na moja ya Paulo. Yaliyomo mambo muhimu katika barua yalikuwa ni mpangilio ndani ya kanisa imani nzima na tabia ndani ya kanisa. Baada ya kuanzishwa kwa kanisa ilikuwa lazima kute­ngeneza mambo ya maka­nisa. Paulo alimfundisha Thimotheo mambo haya.
6:20. Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo; 21. amba­yo wengine wakiikiri hiyo wameikosa Imani. Neema na iwe pamoja nanyi. (1TIM 6:20,21)
TIMOTHEO WA PILI
4:2. Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3. Maana utakuja wakati watakapoya­kataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; 4. nao watajiepusha wasi­sikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. 5. Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. (2TIM 4;2-5)
Hii ni barua ya Paulo ya kumi na tatu na pia ya mwisho. Barua ya kuaga maisha, kwa sababu alijua baada ya muda mfupi atakufa, atau­awa. Alipelekwa tena mara ya pili mbele ya kaisari Nero mwaka wa sitini na saba. Na Paulo alimwuawa.
Makanisa mengine yalikuwa yalipotea kiimani na kuingia chini ya sheria. Paulo alimwomba Timotheo kufanya kazi ya uinjilisti vizuri. Paulo alimhimiza Timotheo aendelee chini ya neema.
TITO
5. Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yali­yopunguka, na kuwe­ka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; (TIT 1:5)
Barua ya Paulo ya kumi na mbili. Tito alikuwa ameachwa kisiwa cha Krete kufanya mipangilio ya kanisa. Paulo aliandika kuhusu mipangi­lio ya ka­nisa na utawala wa kanisa.
Unapotaka kujifunza mambo ya kanisa usome waraka wa Tito na nya­raka za Timotheo.
FILEMONI
1. Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa File­moni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi, ..... 25. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. (FLM 1,25)
Barua ya Paulo ya tisa. Iliandikwa kutoka kifungoni Rumi. Mtumwa kwa jina Onesimo alikuwa amemwibia bwana wake Filemoni na kuto­rokea Rumi. Huko alikutana na Paulo na Onesimo akaokoka. Paulo aliandika ndani ya barua yake ku­husu Onesimo. Alimtetea Onesimo. Onesimo alirudi kwa bwana wake File­moni. Na Paulo alimwandikia Filemoni katika mstari wa kumi na sita: … tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa … (FLM 16)
WAEBRANIA
1. Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2. mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, ali­yemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. (EBR 1:1,2)
Mwandishi hajulikani. Neno kubwa ndani ya barua ni "Afa­dhali". Ba­rua iliandikwa kabla ya mwaka wa sa­bini wakati huo hekalu lilibomo­lewa. Waliopokea hiyo barua ni Wayahudi waliyookoka, waliyoona hekalu kubwa na ibada zilizofanyika humo.
Wakristo walianza kuchoka kwa kumwa­budu Yesu asiyeonekana. Walianza kuyumba ndani ya imani yao. Barua iliwahimiza na kuwakumbusha kwamba kumfuata Yesu ni afadhali kuliko ibada zinazofanyika hekaluni.
13:25. Neema na iwe nanyi nyote. (EBR 13:25)
YAKOBO
1. Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu. (YAK 1:1)
Yakobo alikuwa ndugu yake Yesu, na pia kiongozi wa kanisa la Yeru­salemu na alithaminiwa. Wakati wa utoto alijuana na ndugu yake Yesu na Yuda. Lakini alisema, mimi ni mtumwa wa … Bwana Yesu Kristo.
Inaonekana barua hii ni ya zamani zaidi kuliko barua zote za Agano Jipya. Barua iliandikiwa Wayahudi. Inasemekana kwamba hakuna barua nyingine ya Kiyahudi kama hii.
19. Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; 20. jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi. (YAK 5:19,20)
PETRO WA KWANZA
1. Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawa­nyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia. (1PET 1:1)
Petro anaeleza kuhusu Yesu aliyemwona kwa macho. Barua hiyo ilia­ndikiwa Wayahudi labda mwaka wa 65. Barua inaeleza juu ya mateso na baraka zilizomo ndani ya mateso.
14. Salimianeni kwa busu la upendo. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina. (1PET 5:14)
PETRO WA PILI
1. Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo. 2. Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu. (2PET 1:1,2)
Wazo kubwa ni: Mtu anapokua kiroho analindwa katika wokovu. Petro aliandika waraka huu mwaka wa 66/67.
3:18. Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele. (2PET 3:18)
YOHANA WA KWANZA
1. Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipa­pasa, kwa habari ya Neno la uzima; (1YOH 1:1)
Yohana aliandika barua hii kati ya mwaka wa 85 na 90. Mafundisho ya pembeni yaliingia kani­sani ambayo Yohana anayapinga ndani ya barua yake. Aliendelea kuandika kuhusu dhambi na upatanisho.
18. Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu ha­tendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. 19. Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. 20. Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. 21. Watoto wadogo, jili­ndeni nafsi zenu na sanamu. (1YOH 5:18-21)
YOHANA WA PILI
1. Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote wai­juao ile kweli; ..... 12. Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini nataraji kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa. 13. Watoto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu. (2YOH 1,12,13)
Yohana alitaka kumtahadharisha mama kwa sababu walimu wanao­kosesha walijaribu kuja kanisani. Jina la huyu mama halijulikani na hatu­jui kwamba alikuwa ndani ya kanisa gani. Lakini alikuwa mtendaji kanisani.
YOHANA WA TATU
1. Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. 2. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. (3YOH 1,2)
Yohana alimwandikia Gayo na kumhi­miza atoe msaada kwa wahubiri wana­osafiri.
9. Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali. 10. Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazui­a, na kuwatoa katika kanisa. 11. Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya haku­mwona Mungu. (3YOH 9-11)
Diotrefe alikuwa mchungaji mbaya kani­sani. Hakupenda watu wa ka­nisa wala haku­watunza.
15. Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.(3YOH 15)
YUDA
1. Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo. ..... 25. Yeye aliye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina. (YUD 1,25)
Yuda alikuwa nduguye Yakobo na ndu­guye Yesu. Yuda alimkumbuka Yesu vizuri, walikaa miaka mingi pamoja nyumbani. Lakini Yuda aliandika kuhusu Yesu vi­zuri hivi. Yuda aliandika kuhusu kujilinda na kumfuata Kristo. Inawezekana imeandikwa mwaka wa 66/67.
UFUNUO
1. Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana; 2. aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona. 3. Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuya­shika yaliyo­andikwa humo; kwa maana wakati u karibu. (Ufu 1:1-3)
Yohana aliandika barua hii akiwa kisiwa cha Patino, ambapo Kaisari Domitiani alipomfukuzia. Kaisari Domitiani alitawala mwaka wa 81-96. Yohana aliandika kitabu cha Ufunuo mwaka wa 95. Barua ni ya maono na ufunuo na haina kifani.
Shetani anachukia kitabu hiki cha Ufunuo kwani kina­eleza kuhusu mwisho wake.
Tusingekuwa na Kitabu cha Ufunuo ha­tunge­elewa yanayoendelea sasa. Hatungeelewa ubaya uliomo duniani. Hatungeelewa ni kwa nini Mungu ana­kubali yale yanayotokea dunia­ni. Bila ya Kitabu cha Ufunuo hatungejua mwisho wa dhambi na shetani. Lakini katika Ufunuo tunaambiwa kwamba kila kitu kibaya kina mwisho wake. Bila ya Kitabu cha Ufunuo hatungeelewa ku­husu vita, uhalifu na mateso ma­kali yanayo­wapata wanadamu.
Tukisoma Biblia tangu mwanzo mpaka mwisho tunaona kwamba Ufunuo ni kilele cha mambo yote ya Biblia. Tunaona katika Ufunuo kwamba sha­baha ya Mungu ni nini. Kitabu hiki kinawafariji wanao­teswa na wana­oona mateso ya aina mbali mbali kwa kumfu­ata Yesu.
Pia katikati ya masumbufu ya kila siku, kitabu hiki kinatupa matumai­ni ya mambo yajayo kwamba siku moja hu­zuni zote zitakwisha. Tu­kiangalia huku na huku na kuona uovu una­vyozidi, mateso na kumdhi­haki Mungu, tu­najua kwamba mambo yatabadilika siku moja. Wafuasi wa Yesu watapata thawabu na ma­zuri yajayo. Tunaposoma Ufunuo, tunaona yale ma­zuri ambayo tumeahidiwa na ambako tuko njiani.
1. Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung´aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo, 2. katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, uliku­wapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 3. Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kita­kuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia; 4. nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5. Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele. 6. Kisha akani­ambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za ma­nabii, alimtuma malaika wake ku­waonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi. 7. Na tazama, naja upesi; heri yeye aya­shikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki. 8. Nami Yo­hana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisu­judu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo. 9. Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu. 10. Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa ki­tabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. 11. Mwe­nye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. 12. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, nakuingia mjini kwa milango yake. 15. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. 16. Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung´aa ya asubuhi. 17. Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwe­nye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. 18. Namshuhudia kila mtu ayasikiaye ma­neno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandi­kwa katika kitabu hiki. 19. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. 20. Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema; Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu. 21. Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina. (UFU 22:1-21)