Saturday, October 20, 2012

KISASI


Bwana Yesu Asifiwe,

Natumai kuwa kwa rehema zake Mungu hujambo na unaendelea vyema katika hali na nia ya kumpenda Mungu wetu na kutii maagizo yake ili kuweza fikia ile ahadi yake.
Siku moja nikiwa katika sehemu yangu ya kufanyia kazi, Boss wangu alikujua na kunieleza kuwa kunamwajiriwa mpya atafika punde na niwe tayari kumpokea kwani atakuwa ni msaidizi wangu. Kweli siku iliyo fuatia nilimpokea binti mwenye miaka 22 hivi, alinisabahi kwaheshima zote na Boss naye akanieleza kuwa nimpe ushirikiano wa kutosha.
Siku zikazidi kwenda mbele na tulifanya kazi vizuri tena kwa ushirikiano mkubwa sana, na alidiriki kuniita kaka kwa jinsi nilivyo kuwa namweshimu. 
Alinieleza kuwa kwasababu yeye bado nimchanga kimaisha na ameingia tu katika utafutaji kwa mara ya kwanza, aliniomba nimkosoe pale anapo kuwa amekosea. Kiukweli nilidhamiria tokea moyoni kufanya hivyo na alikuwa akinihadithia mambo mengi sana yahusuyo maisha yake kwani tulikuwa kama ndugu. Kumbe yule binti nilipokuwa nikimkataza kushiriki mambo fulani yasiyo faa kama kuingi kwenye vyumba vyawanaume pasipo sababu maalumu, kwani kwaweza msababishia vishawishi. Pia nilimweleza kuwa ahakikishe anatunza utuwake kwani unathamani kubwa sana mbele za Mungu naye pia, nikiwa nampa mifano iliyohai hususani kupitia mfanyakazi mwenzetu aliyekuwa na mfano mbaya katika suala la uzinzi. Nilimweleza ajitahidi asikubali kurubuniwa kirahisi kwani kijana ambaye nilimtolea mfano wake ameshatelekeza mimba nyingi na anawatoto lukuki wasio kuwa na matunzo. Binti yule alikuwa akinisikiliza kwa makini sana lakini kumbe chini ya kapeti kulikuwa na siri kubwa iliyojificha. Maneno yote niliyokuwa nikimueleza alikuwa akienda tena kumwambia kijana yule mwenye mfano ambaye si mzuri kuuiga. Matokeo yake tukawa hatusalimiani na kijana yule, nilipofuatilia kwanini kijana yule mcheshi tuliezoeana anabadilika na kunipita pasipo kunisalimia, ndipo alipo niambia kuwa iweje niwe namsema vibaya kwa mdada yule ampendaye? N aakaniambia kwa kifupi dada yule nimpenzi wangu na leo fuatilia uone nitaingia kwenyechumba chake na nitatoka asubuhi. Kweli kijana yule aliingia mle ndani kwa yule binti mgeni na akatoka asubuhi yake na ikawa ndio mazoea yao kufanya hivyo. Nikajiuliza kwanini huyu binti aliniomba nimsaidie halafu anafanya haya? Nikataka kumchukia na asinikaribie lakini nikasema nisipo mpenda jirani yangu hata nitakapo sali nitakuwa natwanga maji katika kinu.
Nikampenda yeye pia na kijana wake, nikajipa moyo kuwa hata nimesha nawa mikono sina hatia kwani nilimwelekeza njia ya unyoofu ameikataa. Nikawa na amani moyoni na nikawa naendelea na maisha yangu yakila siku kama kawaida.
Mama yangu mdogo nae alikuja sikumoja kunikopa paesa kwa ahadi kuwaatarudisha, zilikuwa pesa nyingi, alikuja niambia kuwa kachukua mkopo lakini ameshindwa kuulipa hivyo nisipo msaidia atakuwa katika wakati mgumu kwani anaweza filisiwa na anawatoto, mume wake alisha kufa sikunyingi. Kwahuruma nilimkopesha toka 2005 mpaka leo hii hajanirudishia japo kuwa anafanya biashara. Ila baada yakuona amekuwa na moyo mgumu nikaamua kumsamehe tu. Shetani anaweza kupitia mtu ili akuteke nakukuweka katika himaya yake, hivyo hatunabudi kuwa makini sana katika maisha yetu yakila siku.
Kulipisha kisasi ya paswa tumwashie Mungu. Imeandikwa Warumi 12:19 "Wapenzi sijilipizie kisasi bali ipiosheni ghadhabu ya Mungu maana imeandikwa kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa anena Bwana." Mithali 20:22 Yasema "Usiseme mimi nitalipa mabaya mgojee Bwana naye atakuokoa."
Tusilipishe kisasi kwa ajili ya upendo. Imeandikwa, Mathayo 5:38-39 "Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino lakini mimi nawaambia msishindane na mtu mwovu lakini mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie la pili."
Usifurahi adui wako anapo kuwa na taabu. Imeandikwa Mithali 24:17-18 "Usifurahi adui wako aangukapo wala moyo wako usishangilie ajikwaapo Bwana asije akaliona hilo likamkasirisha akageuza mbali naye hasira yake."

No comments:

Post a Comment